Taarifa Kuhusu Moto Unaoendelea Kuwaka Katika Uwanja Wa Ndege wa Jomo Kenyatta Huko Kenya




Timu ya Dharula na Uokoaji Nchini Kenya Imefanya kazi kubwa ya Kuwahamisha Wasafiri na Raia kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kufuatia kuzuka kwa moto Mkubwa Kuanzia Alfajiri ya Leo.



Moto Huo Ulianza majira ya Saa Kumi Alfajiri (04:30 A.m) Umeliathiri sana Jengo la Idara ya Uhamiaji Ingawa hakuna madhara kwa Binadamu yaliyotokea.

Afisa kutoka Jumuiya ya Msalaba Mwekundu wa Kenya Daniel Mutinda Alizungumza na Vyombo vya Habari na Kusema ya Kwamba " Mpaka sasa hatujajua nini hasa kimesababisha moto huu ambao ulianzia maeneo ya watu wanapofikia, Ingawa hakuna madhara Kwa Binadamu lakini Vikosi vyetu vinaendelea na Kupambana na Moto Huo"




Serikali kupitia Idara zake Mbali mbali zinafanya mawasiliano kuhakikisha Abiria wanofika na watakao fika wanaenda kutua kwa dharula katika viwanja vingine vya ndege Hususan Mombasa International Airport (Mombasa) na Eldoret International Air Port.