Tabuley Mklali aliyetamba na kibao cha "Muzinaa" Afariki Dunia


Mkongwe wa muziki wa dansi nchini DR Congo, Tabu Ley amefariki dunia nchini Ubelgiji.

...Alipokuwa amelazwa kabla mauti kumkuta.
Tabu Ley amefariki nchini humo baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa zaidi ya miaka minne.
Mkongwe huyo ndiye mwazilishi wa miondoko ya Sokous iliyoshika chati na kuwa moja ya aina ya muziki uliopendwa zaidi duniani.Alitamba wakati huo pamoja na mwanamama Mbilia Bel ambaye baadaye alihamia nchini Kenya.Baadhi ya albamu zake kali wakati wa uhai wake ni Tompelo, Babeti Sokous, Tete Nakozonga na Muzina ambayo ilikamata ile mbaya.

Vic na Becks wala deal jingine na Vogue



Yeye ni nyota wa miondoko ya muziki wa pop ambaye alijiingiza kwenye ubunifu wa mitindo, na sasa inaonekana kwamba Victoria Beckham yupo mbioni kuingia kwenye uandishi pia.

mwnamke huyo mwenye umri wa miaka 39 alikaribishwa kwenye uhariri wa jarida la Christmas la Vogue Paris, na hakika alihitajika pia kuwepo kwenye kava yake.
Kwenye picha nyingi alizopiga, mama huyo mwenye watoto wanne anaonekana akiwa anauza zaidi kwa mapozi mbalimbali na baadhi ya picha chache akiwa na mumewe David.


Akizungumzia juu ya uamuzi wa wa kumkabidhi majukumu Victoria, mhariri mkuu Emmanuelle Alt alisema: "Tunakabidhi muendelezo wa makala hii kwa mwanamke ambaye, kwa kipindi chote tulichofanyakazi pamoja, amedhihirisha kuwa tofauti kabisa na muonekano wake kwenye jamii.

Helkopta ya Polisi yaanguka juu ya Paa la Bar, Watu wanasa Ndani.


Helcopta ya polisi imeanguka juu ya paa la baa ya Clutha iliyokuwa imejaa wateja usiku wa kuamkia leo jijini Glasgow, Scotland. Mpaka sasa bado kuna watu wamenasa ndani ya baa hiyo na waokoaji wanaendelea kujaribu kuwanusuru watu hao.

KIJANA WA TABORA AJIKATA NYETI ZAKE KUKWEPA USUMBUFU WA "WANAWAKE"


Ayubu Mnazi Alphonce(24) ni kijana ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete akipatiwa matibabu baada ya kuamua kuukata NYETI yake kutumia wembe mpya ili kuepukana na usumbufu anaoupata kutoka kwa wanawake ambao amekuwa nao kimap3nz!...

Imeelezwa kuwa baada ya kutokea mfarakano baina yake na mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika,Ayoub aliamua kuingia ndani na kuukata uume wake kwa kutumia wembe mkali na kisha kuutupa nje..

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa baba mzazi wa Ayubu baada ya kubaini kuwa mtoto wake alikuwa amejifungia chumbani kwa muda mrefu, aliamua kumgongea mlango na alipopata fursa ya kuingia ndani ndipo alipogundua ukweli juu ya jambo hilo na hivyo kumpeleka Ayubu Kituo kikubwa cha Polisi Tabora ambapo jalada la kesi ya kujidhuru lilifunguliwa.

Hata hivyo hali ya Ayubu kwasasa inaendelea vizuri licha ya kuwa amejikata na kubakisha kipande cha sentimeta 5 huku akisubiriwa kufikishwa mahakamani kwa kutenda kosa hilo la kujidhuru mwenyewe pasipo sababu za msingi.

CHANZO: Jamii Forum

BINTI AJIUZA AKIWA NA MTOTO WAKE MGONGONI



OFM ilichukua maelezo pamoja na picha za mnato huku wenzake wakitoka nduki baada ya kuona mwanga wa kamera.

Cha kushangaza, wakati akihojiwa na OFM, Mama K alidai kuwa haogopi  kupigwa picha kwa sababu alishanaswa na kuhojiwa runingani kuhusiana na ishu ya kujiuza hivyo siyo ishu kwake na wala haoni aibu.
Huku akiwa na mwanaye mgongoni, binti huyo alidai kuwa amekuwa akijiuza kutokana na ugumu wa maisha.

OFM: Wewe unatokea maeneo gani na ulianza lini kujiuza?
Mama K: Mimi ni mwenyeji wa Misungwi (wilaya), kwa hapa mjini naishi Mabatini. Sikumbuki nilianza lini lakini yote hii ni kutokana na ugumu wa maisha.
OFM: Huyo mtoto mgongoni ni wa kwako?
Mama K: Ndiyo ni mwanangu wa kumzaa, ana zaidi ya mwaka. Nilijifungua nikiwa na umri wa miaka 15.
OFM: Baba wa mtoto yuko wapi?
Mama K: Sijui.
OFM: Ukipata mteja unamuweka wapi mtoto au unaenda kulala naye na mwanaume?
Mama K: (huku akiondoka) Nawaachia wenzangu.

Katika kujikusanyia data za kutosha, uchunguzi wa OFM uliogusa viunga mbalimbali jijini hapa ulibaini kuwa biashara hiyo haramu imeshika kasi ya ajabu ikihusisha vitoto vidogo kati ya umri wa miaka 12 hadi 16.
Kuhusu bei, tofauti na Dar ambako bei huwa ni ghali, jijini hapa vibinti hivyo vidogo hujiuza kwa kati ya shilingi elfu saba hadi kumi na tano kwa usiku mzima. Hakuna mambo ya ‘short time’.

Akizungumzia na gazeti hili kuhusiana na ishu hiyo ya watoto wadogo kujihusisha na biashara hiyo haramu ya ngono, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo alikuwa na haya ya kusema:“Sina taarifa yoyote kuhusiana na watoto hao wanaojiuza ndiyo nasikia kwako labda unipe muda niongee na uongozi wa chini nitalichukulia hatua mara moja.”

Rihanna Aanguka katika P3nz! la Bwana wake wa Zamani Tena


Inaonekana kama Rihanna huwa hawezi kuwa mbali na waliowahi kuwa wapenzi wake.

Baada ya kufanikisha kwenye kwenye moja kati ya club za usiku za Texas wiki moja iliyyopita, nyota huyo wa muziki wa pop na mpenzi wake wa zamani Drake walionekana kwa mara ningine tena wakiwa wanapati kwenye night club ya Los Angeles.

Wawili hao walipigwa picha wakiwa wanawasili Bootsy Bellows mida ya saa 7 usiku mnamo siku ya Jumanne mara baada ya rapa huyo kutoka kupafomu kwenye tamasha lillilofanyika Staples Center Downtown, taarifa zimesema.

Kiwanja cha Kombe la Dunia 2014 Brazil chaua watatu


Sao Paulo, Brazil - Vifo vya watu watatu vimeripotiwa kutokana na kuanguka kwa sehemu ya kiwanja kitakachotumika kwa ajili ya ufunguzi wa michuano hiyo mnamo siku ya Jumatano, November 27, huku ikielezwa kwamba ajali hiyo pia imesababisha uharibifu mkubwa.

Hii inamaanisha kwamba kutakuwa na ucheleweshwaji wa makabidhiano ya viwanja vyote 12 kwa FIFA itakapofika mwezi Desemba kama ambavyo imepangwa, hii ni kutokana na Uwanja huo wa Itaquerao kuanguka, mpaka inaanguka sehemu ya uwanja huo ulikuwa tayari umekamilika kwa asilimia 94.



  

AMUUA MKEWE NA MIMBA YA MIEZI TISA TUMBONI


JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, linamshikilia Philemon Ng’ambi, mkazi wa Madale Kata ya Wazo, jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumuua mkewe, Enea Kagine kwa kumshambulia kwa mawe na matofali hadi kumuua.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Enea Kagine likibebwa na waombolezaji.
Philemon anadaiwa kufanya unyama huo kwa marehemu mkewe aliyekuwa amebakiza siku mbili kabla ya kujivungua usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita  nyumbani kwake Wazo-Hill.
Akisimulia mkasa huo kwa mapaparazi wetu, jirani wa wanandoa hao aliyejitambulisha kwa jina la Fikiri Rashid alisema:
“Mimi nyumba yangu na yao zinatazamana hivyo siku ya tukio majira ya saa tisa usiku, nilianza kumsikia marehemu akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema mumewe anamuua.
Marehemu Enea Kagine enzi za uhai wake.
“Nilitoka nje kwa lengo la kutaka kutoa msaada lakini nilihofia maisha yangu hivyo ilinibidi niwaite vijana wa ulinzi shirikishi ambao baada ya muda walifika eneo la tukio na kumkuta mtuhumiwa akivunja vyombo vya ndani kama mtu aliyechanganyikiwa, wakati huo tayari alikuwa ameshamuua mkewe.
“Baada ya kuwaona ulinzi shirikishi, alikimbilia chumbani na kwenda kujificha uvunguni kwenye kitanda huku watoto wao watatu wakiwa wamelala.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo, Philemon Ng’ambi.
“Bila kuchelewa, askari wa ulinzi shirikishi walimkamata na kuwasiliana na Askari wa Kituo cha Polisi cha Wazo ambao walifika eneo la tukio na kumtia mbaroni mtuhumiwa pamoja na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya taratibu za kipolisi,” alisema Fikiri.
Mama mzazi wa marehemu Enea akiwa na simanzi nzito.
Kufuatia tukio hilo la kusikitisha wanahabari wetu walifika katika Hospitali ya Mwananyamala ulipohifadhiwa mwili wa mwanamke huyo na mtoto wake waliyemtoa akiwa amefia tumboni.
Miili hiyo ilizikwa Jumatatu iliyopita (Novemba 25) mwaka huu katika kaburi moja kwenye Makaburi ya Madale, Dar es Salaam.
GPL

WATUMIA NYETI ZA MWANAUME KAMA KEKI YA BIRTHDAY


Katika hali inayozidi kuonesha kuporomoka kwa maadili na heshima miongoni mwa wanawake, wasanii fulani nchini Nigeria wamefanya kali ya mwaka pale walipotengeza keki ya Birthday ya rafiki yao ambayo ilipambwa na taswira ya NYETI za kiume ambapo rafiki huyo alikuwa akiilamba kila wakati kama anavyoonekana pichani hapo juu.

MSANII HUYU WA BONGO MOVIE AIVULIA KOFIA NDOA


MSANII wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ amekiri kujifunza mambo mengi ya maisha baada ya kuingia kwenye ndoa.

Halima Yahya ‘Davina’.

Akizungumza na mwandishi wetu, Davina alisema kwamba anaichukulia ndoa yake kama chuo cha mafunzo kwa jinsi alivyobadilika na kuwa tofauti na Davina aliyekuwa nje ya ndoa.

“Nimekuwa tofauti kabisa na Davina wa kabla ya ndoa, sasa hivi kila kitu nakifanya kwa ustaarabu kwa kuwa najiona nimekuwa mwenye majukumu mengi,” alisema.

Akifafanua zaidi, Davina alisema zamani alikuwa ni mtu wa kurandaranda hovyo tofauti kabisa na hivi sasa.
“Zamani nilikuwa napenda safari zisizokuwa na faida tofauti na sasa hivi, kweli nimeamini ndoa ni chuo cha mafunzo,” alisema huku akiwaombea wasanii wenzake walio nje ya ndoa wafunge ndoa na kuwa na familia zao kwani watajifunza mengi.
GPL

MTOTO WA KIGOGO ATUPIA PICHA ZA UTATA MTANDAONI


Imekuwa ni jambo la kawaida na pengine linalochukua sura mpya kwa sasa kutokana na watoto wa vigogo kupiga picha tata yaani za uch! na kuzitundika katika mitando kana kwamba wanajiuza.

Nadani wadau mtakumbuka hapa nchini watoto wengi mastar mbali mbali wa kike wamekuwa na tabia hiyo ya kuanika miili yao katika mitandao haswa BBM na kujinadi kwa wanaume,sina haja ya kuwataja majina hapa maana ni uandikwa wameshaandikwa sana ila bado kila kukicha wanaibuka wengine.


Sasa nchini ghana nako mtoto wa kigogo mmoja ametundika picha zake mtandaoni na kuandika mwenye pesa ananitafute nitamtimizia kila kitu anachokitaka katika mwili wangu,hii inaonyesha hali mbaya sana kwani zaman tulijua watoto wa maskini ndio wanafanya uchafu huo ili kupata pesa ila kwasasa inaonekana watoto wa vigogo wamekuja kwa kasi sana katika swala la kujiuza mitandaoni.


JAMAA WA MIAKA 32 ANSWA NA BIBI WA MIAKA 80, BIBI AWASHUKIA WAJUKUU KWA KUTOMUHESHIMU "BABA YAO" HUYO


KUNA mengi ya kushangaza duniani lakini hili la kijana Hamad Issa (32) kunaswa faragha na bibi kizee Adela Mkalau (80) linaongeza rekodi ya mambo yanayoshangaza, Risasi Mchanganyiko lina kila kitu.
Hamad Issa (32) akiwa amejilaza kitandani kwa bibi Adela Mkalau (80).
Tukio hilo la kustaajabisha limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita, nyumbani kwa bibi huyo, Yombo –Buza, jijini Dar es Salaam ambapo wajukuu wa bibi huyo ndiyo waliomnasa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wajukuu wa bibi huyo walifedheheshwa na kitendo hicho hivyo kuwawekea mtego na kuwanasa kisha kumfikisha Hamad katika Kituo cha Polisi Chang’ombe kwa tuhuma za ubakaji.
Bibi Adela Mkalau (80) akiwa katika pozi.
BIBI: SIJABAKWA
Katika kutafuta uhakika wa madai ya wajukuu hao, polisi wa Chang’ombe waliagiza bibi yao aitwe ili athibitishe madai hayo wakati upelelezi mwingine ukiendelea.
Sosi wetu alisema kuwa bibi aliwaacha hoi polisi baada ya kufika kituoni hapo na kukataa maelezo ya wajukuu zake, huku akisisitiza hakubakwa bali walikubaliana na Hamad.
Baada ya bibi huyo kuondoa utata, polisi walikubali kumuachia Hamad kisha wajukuu wakafunguliwa kesi ya kushambulia na kudhuru mwili iliyoandikishwa kituoni hapo kwa jalada namba CHA/RB/10629/2013.
Hamad Issa akiwa kitandani, pembeni kulia ni bibi Adela Mkalau.
BIBI NA RISASI
Risasi Mchanganyiko lilifunga safari hadi nyumbani kwa bibi huyo na kuzungumza naye kuhusu tukio hilo ambapo alisema: “Sijabakwa na nimekasirishwa sana kwa kitendo cha kumpiga kijana wangu. Wawe na heshima kwa babu yao. Sisi tunapendana, kwa nini wanatuingilia?”
Alisema: “Siku hiyo Hamad wangu alikuja nyumbani kwangu tangu mapema. Nikaandaa chakula cha jioni, tukala pamoja kisha tukalala.
“Tukiwa usingizini, nikasikia mlango unagongwa. Kwenda kufungua, wajukuu zangu wakaingia na kuanza kumpiga Hamad na fimbo na magongo, wakisema eti amenibaka. Hamad atanibakaje? Kwani mimi ni mtoto mdogo?
“Isitoshe wanamfahamu vizuri sana Hamad. Nipo naye  mwaka mmoja na nusu sasa, leo inakuwaje wanajifanya hawamjui? Siku hizi mambo yamebadilika. Mdogo anaweza kumpenda mkubwa na mkubwa akampenda mdogo. Hakuna kosa.”
 akiwa kwa bibi.
MSIKIE DOGO
Mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwa Hamad ambapo alimkuta akiwa hoi kitandani kwa majeraha ambapo alisema: “Ni kweli bibi ni mpenzi wangu... na wale wajukuu zake wananifahamu vizuri sana. Wamenipiga sana, eti nimembaka bibi yao. Siyo kweli. Sisi ni wapenzi.”
Alipoulizwa anajisikiaje kuwa kwenye uhusiano na kikongwe huyo, alijibu: “Hata mimi nashangaa sijui imekuwaje nikampenda. Nimejikuta nipo kwenye uhusiano naye na kwa kweli tunapendana sana.”
WAJUKUU WANASEMAJE?
Mmoja wa wajukuu wa bibi huyo, Margaret Cheba, akizungumza na gazeti hili kuhusu tukio hilo alisema bibi yao amewadhalilisha sana na wanaona aibu kupita mitaani kwa kitendo cha kutembea na Hamad.

“Hili jambo limetufedhehesha sana sisi wajukuu zake halafu hata kimila ni tatizo, hairuhusiwi kabisa. Mbaya zaidi, bibi yetu ni mgonjwa. Anasumbuliwa na moyo... sio wa kufanya kitendo kama kile kabisa na sisi ndiyo tunamsaidia lakini inashangaza polisi wametubadilikia kabisa,” alisema Cheba.

GPL

ATEMBEZWA UCH! MTAANI BAADA YA KUFUMANIWA NA MKE WA KIGOGO WA CCM MTAANI


WANASEMA za mwizi arobaini, ikiongezeka moja mshukuru Mungu! Novemba 16, mwaka huu ilikuwa siku ya aibu kwa bosi Hussein Shaban (35) kufuatia kudaiwa kufumaniwa katika nyumba ya kiongozi mmoja wa Chama cha Mapinduzi (CCM) huko Tegeta jijini Dar es Salaam.
Hussein Shaban akiwa amevuliwa nguo na kupewa kichapo baada ya fumanizi.
Sakata hilo la aina yake lilitokea katika kitongoji cha Nyeishozi, Tegeta kwa kumuhusisha Hussein ambaye ni mfanyabiashara  na mke wa kigogo huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa.
CHANZO CHA FUMANIZI, KUTOWEKA AMANI
Akisimulia tukio zima mwanzo hadi mwisho, kiongozi huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema miezi miwili iliyopita alianza kuhisi ndani ya ndoa yake kuna jambo lanaloendelea kwa siri baada ya nyumba yake kupoteza amani, mke alibadilika tabia ghafla.
Bwana Hussein akitembezwa mitaani.
“Siku moja nilikuwa natafuta nyaraka za kazini ambazo nilikuwa nimeziweka kwenye begi la kubebea kompyuta mpakato (laptop), lakini sikuzikuta.
“Niligundua vitu vyangu vingi havipo ndani kama vile mashati, suruali, redio ndogo na saa ya ukutani. Nilimuuliza mke wangu akanipa majibu rahisi.
UCHUNGUZI WA KINA WAANZA
“Nilianza uchunguzi, niliwahoji shambaboi wangu kuhusu tabia ya mke wangu ambapo waliniambia kila siku nikitoka kwenda kazini nyuma kuna mtu huingia nyumbani kwangu na kukaa na mke wangu kwa muda mrefu ndani.
“Kwa kidokezo hicho, siku moja nilichukua simu ya mke wangu ya kijanjani, nikaipekua na kugundua namba moja ambayo amekuwa akiwasiliana nayo mara kwa mara. Hii namba aliisevu kwa jina la Mwajuma Jumanne.
...Wananchi wakimpiga picha Hussein aliyefumaniwa na mke wa mtu.
“Ajabu ni kwamba, kwa namba hii nilikuta ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wa mapenz kati ya mke wangu na huyo Mwajuma Jumanne. Nilianza kuhisi kuna jambo.
“Moja ya meseji ilisema yeye (Mwajuma) hana mke! Nikajua huyo Mwajuma ni mwanaume niliyeambiwa na shambaboi kuwa huwa anakuja nyumbani kwangu.
“Pia upelelezi wangu uligundua kuwa mwanaume huyo ama huwa anamuibia vitu mke wangu au alikuwa anapewa.
“Niliwahi kuambiwa kuwa kuna siku mke wangu alimpa mwanaume huyo shilingi elfu sitini (60,000/) na akarudia tena hivi karibuni kumpa kiasi hichohicho,” alisema kiongozi huyo.
Hussein akijikinga sehemu za kichwa wakati akipewa kichapo na wananchi.
POLISI WAPEWA TAARIFA
Alisema kufuatia mambo yote hayo, aliamua kwenda Kituo cha Polisi Wazo, Dar kutoa taarifa ya kupotelewa na vitu akimtaja mwanaume huyo kwamba ndiye anayemtuhumu. Kwa ujasiri mkubwa, kiongozi huyo aliwaambia polisi kwamba mtu huyo angemtafuta mwenyewe, likafunguliwa jalada namba WP/RB//7720/2013 WIZI.
MUME AANDAA SAFARI YA UONGO
Akiendelea kusimulia mkasa huo, kiongozi huyo anasema:
“Siku ya tukio, nilijifanya nasafiri kwenda Dodoma kikazi ili kumpa mwanya mgoni wangu kujitawala, niliondoka nyumbani alfajiri huku nikiwa nimeweka wapelelezi wangu.
“Ilipofika saa tano asubuhi, Hussein aliingia nyumbani kwangu na kuanza kujimwaga kama kwake bila kujua arobaini yake ilikuwa inatimia siku hiyo.
...akizidi kutembezwa mtaani.
FUMANIZI LATIMIA
“Mimi na wapelelezi wangu tulivamia nyumba, tukagonga mlango, mke wangu akafungua. Aliponiona ni mimi alianguka kwa kiwewe.
“Nilichungulia ndani kupitia dirishani nikamwona mgoni wangu akivaa shati. Alitoka mbio kuelekea getini. Nilichomoa bastola na kupiga risasi moja hewani, ikampagawisha, akataka kupanda ukuta.
“Nilipiga filimbi watu wakaja, walipojua kisa, walimvua suruali na kuanza  kumpa kipigo huku wakimtembeza mpaka moja ya sehemu anazofanyia biashara zake za kuchemsha supu na kukaanga chipsi, bahati yake aliokolewa na polisi,” alisema kiongozi huyo.
Alipoulizwa alipo mkewe kwa sasa, alisema: “Nilimtimua mbio, kaondoka zake.”
Hussein akiwa ndani ya gari la polisi waliofika kumnusuru.
KAKA WA MTUHUMIWA
Kaka wa damu wa Hussein aliyejitambulisha kwa jina la Tambwe alisema kitendo alichokifanya mdogo wake ni cha aibu ila anapinga adhabu aliyopewa ya kutembezwa uch!.
“Hili tukio alilofanya mdogo wangu ni baya, hata baba yetu mdogo hapa mjini siwezi kumwambia kwa sababu linaweza kumpa presha,” alisema mtu huyo ambaye alimuwekea dhamana polisi mgoni huyo.
Kaka mwingine wa mtuhumiwa, Hamis alisema mama yao mzazi (hakumtaja jina) na bibi yao waliopo Tabora walizimia baada ya kusikia tukio hilo na wameongea kwa simu na mtendewa ili amsamehe mgoni wake.

MKE WA MTUHUMIWA
Mke wa mtuhumiwa, Pili Muhammed akizungumzia fumanizi la mumewe kwa njia ya simu akiwa Rufiji, Pwani alisema: “Mume wangu si mkweli katika mapenz yetu tangu siku nyingi ila niliamua kuvumilia nikiamini atabadilika lakini badala yake sasa amekamatwa ugoni.”
Aliongeza: “Siku ya tukio mtoto wetu mchanga alikuwa anaumwa, nilipomuomba mume wangu anisindikize hospitali aliniambia hajisikii vizuri, akabaki nyumbani kulinda nyumba.
“Niliporudi sikumkuta  na mpaka giza linaingia hakurejea, baada ya muda kidogo nikaambiwa amekamatwa ugoni yupo Kituo cha Polisi Tegeta (si Wazo). Ndiyo nikawapigia simu kaka zake wakaenda kumdhamini.”

GPL

PICHA ZA UTATA ZILICHANGIA MAUAJI YA ILALA, SOMA MKASA MZIMA HAPA



Tukio la Gabriel Munisi kuua watu wawili kisha naye kujiua kwa kisa cha mapenz, ni mwendelezo wa ‘sinema machafuko’ za mapenz.
Nyuma ya tukio hilo kuna mengi yanazungumzwa, ila gazeti hili limenasa habari kuwa picha za utupu na SMS za mapenz ni chanzo cha kila kitu.
Alpha Alfred Newa enzi za uhai wkae.
NINI HASA CHANZO?
Gazeti hili limebaini kuwa tukio hilo la mauaji, lililochukua nafasi alfajiri ya Jumanne iliyopita, chanzo chake ni Gabriel ‘Gaby’, kunasa picha zinazomuonesha mchumba wake, Christina Newa akiwa na mwanaume mwingine.
Habari zinaeleza kuwa Gaby alichukua kompyuta mpakato (laptop) ya Christina na kuikagua, ndipo akakuta picha ambazo mchumba wake huyo alikuwa katika hali ya kustarehe na mwanaume mwingine.
“Kwanza ile laptop ilikuwa inafunguliwa kwa namba za siri (password), ikabidi Gaby awatafute wataalamu wa kompyuta waweze kumsaidia kuifungua.
Francis Shumira enzi za uhai wake.
“Laptop ilipofunguliwa, Gaby aliikagua na kukuta picha ambazo Christina alikuwa ufukweni na mwanaume mwingine.
“Kuanzia hapo, Gaby akawa analalamika kwamba zile picha ni mbaya sana, ni za utupu na kwamba mchumba wake amemfanyia kitendo kibaya sana,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Kama ndugu au hata jeshi la polisi, wangesoma alama za nyakati, pengine yale mauaji yasingetokea maana dalili zilijionesha waziwazi mapema.”
Muuaji Gabriel Munis enzi za uhai wake.
DALILI ZA MAUAJI
Chanzo chetu kilisema kuwa wakati Gaby anaziona picha hizo, alikuwa nyumbani kwake Mwanza, wakati Christina alikuwa Dar es Salaam.
“Kutokana na hali hiyo, Gaby alimpigia simu Christina aende Mwanza. Bila kujua anaitiwa nini, Christina alifunga safari na kwenda Mwanza.
“Christina alipofika Mwanza Gaby alimnyang’anya simu zote mbili alizokuwa nazo, akapitia SMS zote na kubaini kwamba zipo za mapenz.
Mama mzazi wa Alpha akimuaga mwanaye kwa simanzi nzito.
“Gaby akaunga matukio na kudai kwamba mtuma SMS za mapenz ndiye mwanaume anayeonekana kwenye picha na Christina.
“Christina alisema kuwa hakukuwa na ubaya wowote kwa sababu zile picha siyo mbaya ni za ufukweni tu na wanafunzi wenzake,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Utetezi huo haukumsaidia chochote, maana kuanzia hapo aliendelea kupokea kichapo kila mara, kufungiwa ndani na kupewa kila aina ya mateso.”
Christina Newa akilia kwa uchungu.
KILICHOTIBUA NI MASOMO YA ULAYA
Habari zaidi zinasema kuwa Gaby alikuwa anawaambia marafiki zake kuwa kinachomuuma kuhusu Christina ni kumgharamia masomo kwenye Kisiwa cha Cyprus barani Ulaya.
“Alikuwa akilalamika kuwa kama asingempeleka Cyprus kusoma, yote yasingetokea, maana akiwa huko ndiko alipata mwanya wa kujirusha na mwanaume mwingine na kupiga picha alizozikuta kwenye laptop,” kilisema chanzo chetu.
Mwili wa Alpha ukiingizwa kaburini.
Habari zinaongeza kuwa sekeseke zima lilitokea wakati Christina akiwa amerejea nchini kwa likizo.
“Aliporudi nchini aliamua kwenda Mwanza kumsalimia mpenzi wake Gaby, baadaye akaelekea Dar lakini kule Mwanza aliacha laptop ambayo iliibua kasheshe nzima,” alisema mtoa habari wetu.
Mume wa marehemu Alpha, Joseph John akiweka shada la maua kwenye kaburi la mkewe.
DADA ASIMULIA KISA CHA LAPTOP, PICHA NA SIMU
Caroline ambaye ni dada wa Christina, alipozungumza na waandishi wetu, nyumbani kwao, Ilala, Dar, alifafanua kiundani kisa cha laptop, picha na simu, huku akisema kuwa marehemu shemeji yake (Gaby) ni katili.
Caroline, aliye Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), alisema: “Julai mwaka huu mdogo wangu alikuja likizo akitokea chuoni Cyprus. Gaby ndiye alimpokea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na moja kwa moja walikwenda Mwanza bila kupitia nyumbani.
Mama mzazi wa Alpha akiweka shada la maua katika kaburi la mwanaye.
“Baada ya wiki mbili, Christina alimuomba Gaby ampe ruhusa ya kuja Dar kwa ajili ya kumsalimia mama yetu, alimkubalia lakini akamtaka achukue vitu vichache ili asikawie kurudi Mwanza.
Christina akisindikizwa kupeleka shada la maua.
“Christina alikubaliana naye na kuchukua vitu vichache, vingi aliviacha ikiwemo laptop aliyokuwa anatumia chuoni. Alipoondoka Gaby alichukua laptop yake na kuipeleka kwa fundi ili amfungulie kwa sababu ilikuwa na password, alipofanikiwa alikutana na picha zinazomuonesha Christina akiwa amevaa nguo za kuogelea,” alisema Caroline.
Ndugu na jamaa wakiaga mwili wa marehemu Gabriel Munisi.
Hata hivyo, Caroline alipingana na madai kuwa Christina alipiga picha za utupu na mwanaume mwingine, badala yake alisema:
“Christina alipiga akiwa beach na wasichana wenzake huko Ulaya na hazikuhusiana na suala la kimapenz.”
Caroline akaendelea: “Gaby hakusema kilichokuwa kinaendelea badala yake alimpigia simu na kumtaka arudi Mwanza kwani amemkumbuka. Alimkatia tiketi ya ndege na kumtumia, kweli Christina akaenda Mwanza.
“Kufika Mwanza ndiyo ugomvi ulianza. Gaby alimnyang’anya Christina simu zake mbili kisha akaanza kumpiga huku akiwa amemshikia bastola.
Mwili wa Gabriel Munisi ukiingizwa kaburini.
“Christina alimwambia Gaby kuwa kama kupiga picha na nguo za ufukweni ni tatizo basi wawasiliane na mama yetu mzazi, naye aseme maana ndivyo tulivyolelewa lakini hakuelewa.
“Gaby alimfungia ndani Christina na kumpa mateso makali ambayo yalimsababishia majeraha na kudhoofu mwili. Aliendelea kuteseka bila kutujulisha ndugu zake, maana simu zote Gaby alizishikilia.
“Kila SMS iliyoingia, alipokea na kuijibu akijifanya yeye ndiye Christina. Kutokana na mateso kuzidi kuwa makali, Christina alishauri waende kwa wazazi wa Gaby kwa usuluhishi lakini kule nako hawakusuluhishwa, baba yake Gaby alisema wavumiliane kwani hayo ni mambo ya mapenz.
Wazazi wa marehemu wakiweka udongo.
“Akiwa amefungiwa ndani, siku moja Christina alipanda dirishani na kumuona kaka mmoja akipita barabarani, akamwita, akamtajia namba ya simu ya mama yetu ili awasiliane na amwambie jinsi anavyoteseka.
“Yule kijana alipiga simu, baada ya taarifa kufika kwetu ilibidi tuongee na askari wa Kituo cha Polisi Kitangiri lakini wakatujibu hawaingilii mapenzi ya watu.
“Baadaye Christina alifanikiwa kuzungumza na watoto wa mwenye nyumba ambayo Gaby alipanga ambayo ndiyo Christina alifungiwa ndani, akaomba msaada wa kuokolewa.
Christina Newa akiwa hospitali baada ya kujeruhiwa na mpenzi wake.
“Mama mweye nyumba alimpigia simu mumewe ambaye naye alimpigia Gaby, akamwambia amepata taarifa kuhusu Christina, akamweleza kama wameshindana bora waachane kuliko kumtesa.
“Gaby alikanusha, akasema hayo maneno hayana ukweli. Hata hivyo mateso yaliendelea, kitendo kilichotufanya tumweleze ndugu yetu mwingine anayeishi huko Mwanza atoe taarifa polisi, askari hao walienda na kumchukua Christina na Gaby hadi kituoni. Hiyo ilikuwa Agosti 14, mwaka huu.
“Agost 17, Christina alirejea Dar huku akiwa hana chochote, maana kila kitu kilibaki kwa Gaby. Baada ya hapo tukasikia Gaby alikuwa anazunguka kule Mwanza kwa marafiki zake na ile laptop, akionesha zile picha za Christina.
“Tukasikia Gaby anatangaza kwamba ataua familia yetu yote, sisi tulitoa taarifa Kituo cha Polisi Pangani. Kumbe Gaby alikuja Dar na kupanga kwenye Hoteli ya MM ambayo inapakana na nyumba yetu.
Gabriel Munisi baada ya kujiua kwa risasi.
“Kwa maana hiyo, akiwa ghorofani akawa anatazama kila kilichokuwa kinaendelea kwenye nyumba yetu.
 “Gaby akawa anampigia simu Christina kumuomba msamaha. Christina akamjibu atafute kwanza daktari wa saikolojia amtibu, kisha baada ya miezi mitatu ndipo watarudiana. Akamshauri pia aende kanisani akatubu kwa dhambi alizomfanyia. Gaby alikubali.
“Jumanne iliyopita ambayo ndiyo siku ya tukio, ilikuwa ndiyo siku ya Christina kwenda chuoni Cyprus. Basi akawa anasindikizwa na mama, Alpha ambaye ni mdogo wetu wa kike na mume wangu, Kapteni Francis Kiranga, walipofika getini walimwona Gaby anakuja upande wa getini, alipowakaribia, alichomoa bastola. Mume wangu (Francis)  alipomuona, alishuka kwenye gari kwenda kumzuia asifanye jambo lolote baya.
“Bahati mbaya Gaby alianza kumshambulia mume wangu kwa risasi tano, kisha akampiga Alpha na Christina kabla ya kujilipua mwenyewe.
Kulia ni ambulance ikiwakimbiza majeruhi hospitali baada ya kupigwa risasi na Gabriel.
VIFO BILA HATIA
Mungu ana siri kubwa sana, maana pengine dhamira ya Gaby ilikuwa kumtoa uhai Christina lakini mhusika akapona, ila wasio na hatia ndiyo waliaga dunia.
Francis ambaye ni mume wa Caroline alifariki dunia siku mbili baada ya tukio akiwa Hospitali ya Taifa, Muhimbili wakati Alpha, mauti yalimkuta eneo la tukio, huku Christine na mama yake, wakipata majeraha ya risasi na mpaka sasa wanaendelea na matibabu.
MUNGU AWALAZE PEMA MAREHEMU
Marehemu Alpha aliagwa Jumamosi iliyopita, nyumbani kwao Ilala, Dar es Salaam kisha kusafirishwa kwenda Goba, Bagamoyo kwa mazishi.
Mwili wa Francis, unatarajiwa kusafirishwa leo Jumanne kwenda kwao Nairobi nchini Kenya.
Ndani ya gari walilokuwemo marehemu na majeruhi.
MWANZA WAMZUNGUMZIA GABY
Habari zinasema kuwa maisha ya Gaby kwa jumla yalikuwa ya kibabe na alikuwa mwepesi kuchomoa silaha kumtishia mtu aliyegombana naye.
“Tuliwahi kumnyang’anya bastola mara tatu, sijui kwa nini alikuwa anarudisha ile silaha yake,” kilisema chanzo chetu ndani Kituo cha Polisi Kati, Mwanza.
Hata hivyo, wapo ambao walisema Gaby alikuwa mtu mzuri na wanashangazwa na tukio zima lilivyotokea.
TAHADHARI YA WANAWAKE
Gaudencia Eliona (si jina lake halisi) ambaye amejitambulisha kuwa ni mke wa mtu, alisema kuwa matukio ya wanaume kuua kwa visa vya kimapenz, yanaibua mengi ambayo yanafichika kwenye nyumba nyingi.
“Binafsi sina amani kabisa, mume wangu kila mgogoro kidogo anatishia kunipiga na bastola,” alisema Gaudencia na kuongeza:
“Mume wangu anao marafiki zake wanne, wote wanamiliki bastola, wawili kati yao ni wakorofi sana kwa wake zao. Jamani tunateseka, tunaishi roho mkononi.
“Katika hao marafiki wawili wakorofi, siku mmoja wao alikorofishana na mkewe, akamtishia kumpiga risasi, baadaye akaweka bastola chini ya mto, basi siku hiyo yule mke wake hakulala kwa woga.”
Wanausalama wakikagua gari lililoshambuliwa kwa risasi.
USHAURI KWA SERIKALI
Wakili maarufu na aliye pia Mwenyekiti wa Zamani wa Chama cha Wanasheria Tanzania, Constantine Mutalemwa, alisema kuwa anashangazwa na taratibu zinazotumika ili mtu kuweza kumiliki silaha.
 “Umefika wakati kuangalia upya sheria ya umiliki silaha nchini, kwani baadhi ya wamiliki wamekosa elimu ya matumizi ya silaha,  hivyo kusababisha matukio ya mauaji ambayo siku za hivi karibuni yamekuwa yakiongezeka,” alisema Mutalemwa.
NI KAMA UFOO SARO
Tukio la Gaby, limekuja ikiwa bado Watanzania wanakumbuka lile la Anthery Mushi, kumpiga risasi mchumba wake Ufoo Saro na mama yake, Anastazia Saro kisha naye kujilipua na kufa papo hapo.
Katika tukio hilo, Ufoo alipona, huku Anastazia akifariki dunia.
Imeandikwa na Gladness Mallya, Makongoro Oging’, Issa Mnally, Dar es Salaam na Mashaka Baltazar, Mwanza.