AVULIWA NGUO NA KUBAKI NA "CHUP*" BAADA YA KUMUIBIA BUZI LAKE SIMU NA KUIFICHA KUAKO NYETI, ACHEZEA KICHAPO CHA MBWA MWIZI

Stori: Richard Bukos na Makongoro Oging'
MREMBO mmoja mkazi wa Mabibo Makutano jijini Dar es Salaam (jina lake halikupatikana) mwishoni mwa wiki iliyopita alinusurika kifo baada ya kuvamiwa na kudundwa baada ya kudaiwa kukwapua simu ya mwanaume na kuificha sehemu zake za siri.

Mrembo akiwa chini baada ya kuchezea kichapo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, awali mrembo huyo alikuwa akila bata na mwanaume aitwaye Hashim kwenye Baa ya Jassun Inn iliyopo maeneo ya Mabibo huku mwanaume huyo akiwa ametandaza simu zake za kisasa juu ya meza.
Imedaiwa kuwa wakati wakiendelea kuponda raha, Hashim alikwenda msalani kwa lengo la kujisaidia na kuacha simu zake mezani, aliporudi hakumkuta mrembo aliyekuwa akiponda naye raha na simu yake moja haikuwepo.
...Akiwa amewekwa mtu kati na wananchi.
“Jasho lilimtoka Hashim na kuwauliza watu waliokaa jirani alikoelekea mrembo huyo,” alisema shuhuda mmojawapo wa tukio hilo na kubainisha kwamba msamaria mwema mmoja alimweleza Hashim mwelekeo wa mrembo huyo.
Bila kuchelewa Hashim aliwakusanya wapambe wake na kuanza kumtafuta mrembo huyo na wakamnasa mita kama 150 kutoka Baa ya Jassun na kumuuliza kuhusu simu iliyokuwa mezani lakini alileta ubishi.
“Walijitahidi sana kumbembeleza ili aitoe simu kwa hiyari yake lakini alikataa, ndipo Hashim na wapambe wakamwanzishia songombingo la nguvu na kufikia kumvua nguo hadharani na simu ikakutwa kwenye nguo yake ya ndani,” shuhuda wetu alisema.



Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, hadi kufikia kupatikana kwa simu hiyo, mrembo huyo alikuwa hoi kutokana na vurugu aliyofanyiwa na wapambe wa Hashim ambao walipoipata simu walimvisha nguo pamoja na wigi lake lililokuwa limemvuka.

GPL

MASTAA W BONGO MOVIE MAMPONDA WEMA SEPETU BAADA YA KUNYANG'ANYWA KILA KITU NA MP#NZI WAKE KIGOGO WA SERIKALINI.


MASTAA wa kike Bongo wamecharuka na kutoa yao ya moyoni baada ya nyota mwenzao, Wema Sepetu kubwagwa na aliyekuwa mpenzi wake, anayetambulika kwa jina moja la Clement na kumnyang’anya vitu alivyompa kama zawadi wakati wa mapenzi yao.
Wema Sepetu.
Kuhusu Wema kuporwa ofisi yake ya Endless Fame Film Production, kupewa notisi ya nyumba aliyokuwa amepangiwa na kigogo huyo anayeelezwa yupo serikalini na kunyang’anywa magari siyo stori kabisa mjini.
Risasi Mchanganyiko lilifanya mahojiano na mastaa hao wikiendi iliyopita, kwa njia ya simu na kuwahoji kuhusu kitendo alichofanyiwa mwenzao ambapo walifunguka bila wasiwasi wowote.
USENGENYAJI
Wakali hao, waliopata kuzungumza na waandishi wetu kwa nyakati tofauti, baadhi wamemponda Wema kwa kutokuwa makini wakati akiwa kwenye uhusiano na kigogo huyo kwa kutaka kukabidhiwa hati za vitu alivyopewa.
Wa kwanza kuzungumza ni Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye alisema: “Mimi namshukuru Mungu kwa sababu sijapangiwa nyumba na mwanaume.  Naishi maisha yangu simpo ya furaha na amani, sipendi kuigiza maisha. Hao wasanii wanaopenda mambo makubwa wakati hawana uwezo,  nawashauri wafanye kazi, filamu zinalipa sana. Wasipende vitu vya haraka, maana siku zote vizuri huja taratibu.”
ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’
“Mastaa tusijiachie sana kwa wanaume, kama ukipewa gari, upewe na kadi... tusidanganyike na tusipende kuhongwa, tutafute vya kwetu. Kama mtu anakupenda na anakusaidia kwa mapenzi mema, sawa mheshimu.”
WASTARA JUMA
“Inabidi tujitambue jamani, maana kuna watu wanatembea na mastaa makusudi ili wajulikane au kwa manufaa yao wenyewe. Tuache kuishi kwa kutegemea migongo ya wengine. Wengi hawana mapenzi ya kweli. Hata kama mmeachana, sasa kuna sababu gani ya kumnyang’anya mtu vitu ulivyompa?”
NURU NASSOR ‘NORA’
“Mimi najisikia vibaya sana... kama mtu unajiamini una kipaji, kwa nini usifanye kazi?  Mastaa tuache kujitangaza, kwa sababu tunatumika kama vyombo vya starehe tu.  Tutafute ndoa, tusitumie ustaa kufanya ufuska kwa sababu mali zinapita na mwisho wa siku tunaharibu maisha yetu.”
TAMRINA POSH ‘AMANDA’
“Utapeli ni mwingi, haya mambo ya kupewa vitu siyo vizuri kabisa, tuache.  Wanawake tuna akili fupi sana na tunajisahau tunapokuwa na wanaume wakati wenyewe wana kitu moyoni mwao, akishapata anachotaka anaanza matatizo.



“Bora nitembelee taksi au Bajaj kuliko kudhalilishwa... wanawake ni wajinga na huwa tunajidanganya kwa vitu visivyo vyetu, mwisho wa siku tunaumbuka. Tuache sifa za kijinga.”

MBALI NA KUPENDEZA NA KUVUTIA, BEYONCE AANIKA "NYETI" ZAKE HADHARANI ALIPOANZA KUPIGA SHOW JUKWAANI.


Bila kupoteza muda, picha zinajieleza, maana Beyonce alipata bahati ya kutumbuiza pamoja na mumewe,sasa basi katika songombingo za hapa na pale jukwaani, lol, kumbe kigua alichokivaa kinaonesha maumbile yake wazi, ni hatari


Angalia picha ya hatari zaidi hapo chini, yaani kila kitu wazi kabisa. Hii nini sasa?!! Mimi sisemi.




RAYUU ATAMANI AOLEWE NA KINGWENDU


MSANII wa kike wa filamu Bongo Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amefunguka kwa kusema kuwa mwanaume sahihi kwake na anayestahili kumuoa ni Rashid Mizengwe ‘Kingwendu’ kwa kusema anaamini ndiye anaweza kuwa mwaminifu na kuishi naye kwa raha tofauti na mwanaume mwingine yoyote endapo atapata bahati ya kuolewa naye.

“Unapofika umri fulani suala la kuolewa si mjadala bali ni lazima iwe hivyo lakini shida inakuja je utaolewa na mwanaume anayekujali, kuheshimu na kukupenda? Basi kwangu nataka kuolewa na mwanaume kama Kingwendu naamini nitakuwa na amani raha mstarehe, tofauti na kama nitapata sharobaro sina hakika kama atanijali,”anasema Rayuu kwa fulaha.
Rayuu alisema hayo alipoongea na Maskani Bongo katika mahojiano yake na gazeti hili kuhusu mume gani bora kwake na angependa kuolewa naye na kuishi kama mke na mume, msanii alisema kuwa anahitaji mtu aliyetulia sambamba na umri wa makamo na mtu anayempenda sana kama awe mumewe ni msanii mwenzake Kingwendu au anayefanana nae.