Aliyefumaniwa Ashindwa Kesi

Mwanamke mmoja, Portia Jowa, Raia wa Malawi, ambaye alifumaniwa na aliyekuwa mumewe katika lodge moja akiponda raha na kijana mmoja, ameshindwa kesi aliyoifungua mahakamani akidai fidia ya $420, kama gharama za matunzo ya kila mwezi, hata hivyo mumewe huyo aliiomba mahakama impunguzie kiasi hicho na kushangaa kwanini ampe matunzo wakati watoto hao 3 anaishi nao yeye(mume), mbele ya hakimu Tatenda Manhanzva. Hakimu huyo aliitupilia mbali kesi hiyo na kumshauri mama huyo aanze na kufungua upya kesi ya kuwaomba watoto kisha ndo adai matunzo.